Klabu ya Azam Fc imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Franck Tiesse. kutoka Stade Malien (Mali)
Taarifa iliyotolewa na Azam Fc, imethibitisha kukamilika kwa usajili huo
"Tumefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) ya kumsajili kiungo mshambuliaji wao, Franck Tiesse.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili atakaoanza kuutumikia kuanzia msimu ujao 2024/25.
Tiesse anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu"