Yanga - Local - Transfer

Yanga yajipanga kumbakisha Aziz Ki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2024
Yanga yajipanga kumbakisha Aziz Ki

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewahakikishia Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu ujao wataendelea kuwaona wachezaji wao bora kikosini wakiwemo wale ambao mikataba yao inaelekea ukingoni

Wananchi bado hawana uhakika kama mchezaji wao bora wakati huu Stephane Aziz Ki na mlinda lango Djigui Diarra wataendelea kuwa sehemu ya kikosi hasa ikizingatiwa mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Aziz Ki anatajwa kupokea ofa kutoka timu za hapa Tanzania, Afrika na hata nje ya Afrika, klabu zenye misuli ya pesa kama Mamelodi Sundowns na hata Al Ahly nazo zikitajwa kuiwinda saini yake

Kamwe amesema pamoja na mazingira hayo, anaamini Aziz Ki ataendelea kuitumikia Yanga kama ilivyo kwa wachezaji wengine ambao kocha Miguel Gamondi anahitaji kuendelea nao

"Aziz Ki ni kweli anamaliza mkataba wake lakini kwa hapa Tanzania sioni kama kuna timu ambayo anaweza kucheza tofauti na Yanga"

"Aziz anahitajika na timu nyingi, kwa hizi timu za Afrika Kusini Aziz hawezi kucheza na watu wanaofanya dhuluma namna ile"

"Ziko ofa nyingi lakini kubwa ambalo naweza kuwaambia wanayanga, wachezaji bora ambao wamewaona kwenye kikosi chetu wanasalia kwenye kikosi chetu," alisema Kamwe

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’