Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kinarejea jioni ya leo kutokea Arusha baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu Fc jana na kutinga fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB
Kamwe amesema kikosi kitafanya mazoezi Arusha. Jumanne asubuhi Yanga itaelekea Dodoma kuikabili Dodoma Jiji May 22
Katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji siku ya Jumatano, Yanga itapata heshima 'guard of honor' kwa kutwaa ubingwa mapema
Hii itakuwa mechi maalum ya kushukuru benchi la ufundi kwa kuhakikisha Yanga imetwaa ubingwa wa 30. Itakuwa 'Gamond Day'
Katika mchezo huo itakapofika dakika ya 30, mashabiki wote watasimama kumpigia makofi Gamondi na benchi lake la ufundi kwa kazi nzuri ya kuipa Yanga ubingwa wa 30
Wale watakaoweza kutengeneza picha ya Gamondi, watasimama nayo katika dakika ya 30
May 23 Yanga imealikwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk Damas Ndumbaro kuhudhuria Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kikosi cha Yanga kitarejea jijini Dar es Salaam jioni ya May 23 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Tabora United
May 25 Yanga itakabidhiwa ubingwa katika mchezo dhidi ya Tabora United utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga imetangaza May 25 ni siku ya kibingwa kwa mashabiki wa Yanga kuelekea uwanja wa Benjamin Mkapa kwenda kukabidhiwa taji la ligi kuu ambalo wataondoka nalo moja kwa moja
Mageti ya Benjamin Mkapa yatafunguliwa saa 5 asubuhi tayari kwa mashabiki kuingia uwanjani. Kutakuwa na burudani za muziki kutoka kwa wasanii wakubwa wa ndani na nje ya nchi
Lakini pia, kutakuwa na suprise kubwa itashuhudiwa saa 5 asubuhi katika jiji la Dar es salaam
Viingilio VIP A - SOLD OUT, VIP B - Tsh 10,000/-, VIP C - Tsh 5,000/- na Mzunguuko - Tsh 1,000/-
Baada ya mchezo kumalizika, sherehe za ubingwa ndio zinaanza rasmi, kutakuwa na mkesha wa ubingwa!
May 26 kombe litaondoka dimba la Benjamin Mkapa kuelekea Jangwani yalipo Makao Makuu ya Yanga. Hivyo Parade la Ubingwa mwaka huu litaanzia Benjamin Mkapa kuelekea Jangwani
Kabla ya Parade saa 2 asubuhi Wananchi wakakunywa supu ya ubingwa pale kwa Mkapa ambapo mpaka sasa tayari ng'ombe 11 wameandaliwa
Baada ya supu parade la ubingwa kuelekea Jangwani itaanza rasmi kupitia barabara maalum zitakazotangazwa