Simba yaomba sapoti ya mashabiki

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th May 2024


Simba yaomba sapoti ya mashabiki

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Mgunda amesema shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani hivyo wanawahitaji sana katika mechi hizi za kuhitimisha msimu ili kuweza kutimiza malengo yao

"Tumefanya maandalizi mazuri na tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Geita Gold utakaopigwa hapo kesho"

"Tunawaheshimu Geita Gold, ni timu nzuri ambayo ina kocha mzuri lakini niseme tuko tayari kupambana na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri"

"Katika mchezo huo tutaingiza wachezaji 11 kutuwakilisha lakini tutahitaji nguvu ya mchezaji wetu muhimu wa 12 ambaye ni shabiki"

"Hivyo niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuwaongezea hamasa wachezaji na kuhakikisha wanashinda mchezo huu," alisema Mgunda

Simba inazihitaji alama tatu katika mchezo huo pamoja na mechi nyingine mbili zitakazokuwa zimebaki ambazo zote zitapigwa uwanja wa Azam Complex


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.