Simba - Local - KMC

KMC yagomea mechi dhidi ya Simba kupigwa Arusha

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 May 2024
KMC yagomea mechi dhidi ya Simba kupigwa Arusha

Klabu ya KMC imedai kuwa haitambui mabadiliko ya uwanja wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumamosi May 25 2024

Msemaji wa klabu hiyo Khalid Chukuchuku amesema kulingana na kanuni za ligi, taarifa ya mabadiliko ya uwanja ilipaswa kutolewa siku saba kabla ya mchezo husika

Chukuchuku amesema KMC ilitaarifiwa Jumamosi iliyopita kuwa mchezo kati yake na Simba utapigwa uwanja wa Meja Jen. Isamuhyo hivyo hawatambui mabadiliko hayo kwa kuwa yako nje ya muda uliotajwa kikanuni

"Ukisoma kanuni zinakwambia taarifa ya mabadiliko ya uwanja inatakiwa itolewe siku 7 kabla ya mchezo, Jumamosi iliyopita tulipewa taarifa mchezo utachezwa Katika Uwanja wa Meja Jenerali isamuhyo"

"Zimebakia siku tatu kabla ya mchezo tunaona taarifa kuwa kuna mabadiliko ya uwanja kanuni zimevunjwa sisi tunajiandaa kucheza mchezo wetu katika uwanja wa Isamuhyo"

"Ukisema kwamba Dar es salaam siku hiyo viwanja vitakuwa vimejaa ni uongo siku ya Jumamosi uwanja wa Isamuhyo utakuwa hautumiki kwa sababu JKT Tanzania watakuwa Tanga dhidi ya Coastal Union, Lazima tuzingatie kanuni zilizowekwa, " alisema Khalid

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
23m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
35m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
9h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’