Transfer - International

Tetes za usajili Ulaya, Alhamisi May 23 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 May 2024
Tetes za usajili Ulaya, Alhamisi May 23 2024

Klabu mpya iliyopanda daraja inajaribu kumshawishi meneja wao kusalia, wakati Mauricio Pochettino akiwa na chaguzi kadhaa mezani za kuamua atakokwenda.. Ipswich imempa meneja Kieran McKenna mkataba mpya ulioboreshwa kwa matumaini ya kusalia naye huku kukiwa na nia ya Manchester United , Chelsea na Brighton kumchukua (Sun)

Chelsea wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa McKenna kuhusu kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 kuwa meneja wao mpya. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 29, anaweza kuondoka msimu huu ikiwa Manchester City itapokea ofa ya takriban £50m. (Football Insider)

Uingereza inaweza kumteua meneja wa zamani wa Chelsea Mauricio Pochettino ikiwa Gareth Southgate ataondoka wadhifa wake baada ya Euro 2024. (Telegraph - usajili unahitajika)

Muargentina Pochettino, 52, angependa kuzungumza na Manchester United iwapo watamfuta kazi meneja Erik ten Hag (Times)

Chelsea imeunda orodha fupi ya wagombea wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Pochettino na wanatarajia kufanya uteuzi baada ya siku chache (Athletic)

Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, anatazamiwa kukataa ofa kutoka klabu za Paris St-Germain na Saudi Arabia huku akitarajia kuhamia Chelsea(Teamtalk)

Arsenal wako tayari kumnunua kipa wa Feyenoord na Uholanzi Justin Bijlow, 26, huku wakitarajia mlinda lango wao wa England Aaron Ramsdale, 26, kuondoka.(Mirror)

Tottenham wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 27, ili kutoa nafasi kwa mshambuliaji wa Uingereza na Bournemouth Dominic Solanke, 26. (Talksport)

Wawakilishi wa mchezaji wa Manchester City Kevin de Bruyne walifanya mazungumzo na klabu mpya ya MLS San Diego FC , lakini hakuna daalili kwamba kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji, 32, yuko tayari kuhama(Athletic)

Crystal Palace wameafikiana na beki wa kati wa Morocco na Real Betis Chadi Riad, 20, katika mkataba wa thamani ya hadi £14m(Standard)

Kipa wa England Jordan Pickford, 30, ametoa ishara za wazi kwamba atasalia na Everton licha ya kuivutia Chelsea.(Mirror)

Mkurugenzi wa michezo wa Crystal Palace Dougie Freedman, 49, amekataa ofa kutoka kwa Newcastle United kuchukua nafasi ya Dan Ashworth katika nafasi kama hiyo na atasalia na The Eagles. (Football Insider)

Mshambulizi wa Slovenia Benjamin Sesko, 20, ambaye yuko kwenye rada ya Chelsea na Arsenal , ataamua kabla ya michuano ya Euro ikiwa anataka kusalia RB Leipzig au kuondoka. (Fabrizio Romano)

Newcastle wanakaribia kuwasajili wachezaji wawili wa safu ya ulinzi ya Uingereza Tosin Adarabioyo, 26, na Lloyd Kelly, 25, ambao watakuwa wachezaji huru wakati mikataba yao katika klabu ya Fulham na Bournemouth itakapotamatika msimu huu, huku Eddie Howe pia akimtaka fowadi wa Crystal Palace Michael Olise, 22, ingawa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa kikosi cha wachezaji chini ya miaka 21 anamezewa mate na vilabu vingi(Teamtalk)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’