Rais wa heshima klabu ya Simba Mohammed Dewji ambaye pia ni Mwekezaji wa klabu, ameahidi kufanya mabadiliko katika uongozi kuelekea zoezi la kuijenga upya Simba
Aliyewahi kuwa Mtendaji wa klabu hiyo Barbara Gonzalez jina lake limetajwa sana na Wanasimba wakipendekeza arejeshwe kuchukua nafasi ya Imani Kajula ambaye Simba huenda isimuongezee mkataba pale mkataba huo utakapomalizika
Taarifa kutoka mtu wa karibu wa Barbara, amethibitidsha kuwa Barbara yuko tayari kurejea tena kuiongoza Simba anachosubiri ni wito wa Mo tu
Barbara alijiengua Simba baada ya msimu wa 2022/23 kumalizika kutokana na sababu za kifamilia
Aidha taarifa zaidi kutoka ndani ya uongozi imebainisha kuwa Simba itawaruhusu wachezaji wanaotaka kuondoka kwa kuzingatia taratibu na pia itaachana na wachezaji ambao hawakidhi mahitaji ya klabu
Kulingana na Mwanahabari maarufu wa Ghana Micky Junior, miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakapewa mkono wa kwaheri na Simba ni pamoja na Saido Ntibazonkiza, Luis Miquissone, Jobe Pa Omar, Freddy Michael, Sarr Babacar, Hennock Inonga Baka na Aishi Manula