Yanga - Local - Transfer

Kamwe atamba kuhusu usajili Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jun 2024
Kamwe atamba kuhusu usajili Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa katika usajili wa dirisha hili watashusha wachezaji bora na wenye majina makubwa

Baada ya msimu kuhitimishwa shauku ya kila Mwananchi ni kufahamu mikakati ya kuelekea msimu ujao wengi wakisubiri kwa hamu taarifa za usajili

Msemaji huyo wa Yanga amesema kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa akiwahakikishia Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuwa furaha yao itaendelea hata pale dirisha la usajili litakapofunguliwa

"Uongozi unasubiri ripoti ya benchi la ufundi kuhusu wachezaji ambao watahitaji kuendelea nao pamoja na maboresho kuelekea msimu ujao"

"Niwaambie tu, kama alivyosema Rais wa Yanga Injinia Hersi Said, msimu ujao tumeweka malengo makubwa hasa kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa"

"Hivyo wachezaji wote ambao benchi la ufundi litapendekeza tuendelee nao msimu ujao watabaki. Tukiwa timu yenye malengo ya kuliteka soka la Afrika, lazima tuhakikishe wachezaji wetu bora wanabaki"

"Lakini pia tutafanya maboresho ambayo yataendana na mahitaji ya malengo tuliyoweka msimu ujao. Katika usajili uliopita tulileta wachezaji wenye 'quality' lakini hawakuwa na majina makubwa. Safari hii tunashusha wachezaji wenye quality lakini pia wana majina makubwa," alitamba Kamwe

Aidha Kamwe amesema ile ahadi ya usajili wa mchezaji ambaye bango lake litawekwa mkabala na yalipo Makao Makuu ya klabu moja hapo Kariakoo, itatekelezwa

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’