Yanga - Simba - Azam - Local

Stars kuifuata Zambia Jumamosi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jun 2024
Stars kuifuata Zambia Jumamosi

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kitaondoka nchini kesho kuelekea Zambia kwa ajili ya kucheza mechi ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2026

Zambia maarufu Chipolopolo itaikaribisha Taifa Stars katika mechi ya Kundi E itakayochezwa Jumanne kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa ulioko katika Mji wa Ndola

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema jana kikosi cha timu hiyo kimekamilika baada ya nyota ambao walikuwa katika majukumu ya klabu zao kuripoti

"Kikosi cha Stars sasa kimekamilika, wachezaji wote walioitwa wamewasili, na leo (jana), wamefanya mazoezi kwa Mkapa na kesho (leo), wataendelea kujinoa hapo, wanajiimarisha kwa ajili ya kuhakikisha wanapata matokeo bora huko Zambia," alisema Ndimbo

Aliongeza benchi la ufundi la Stars lililoko chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Hemed Morocco, limeridhishwa na viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji katika michezo ya kirafiki iliyofanyika Indonesia wiki iliyopita

Tanzania inaburuza mkia katika Kundi E ikiwa na pointi tatu sawa na vinara Morocco, Zambia na Niger, hii inatokana na tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’