Yanga - Simba - Azam - Local

Kagame Cup kuanza Julai 06

Joel JJ By Joel JJ
11 Jun 2024
Kagame Cup kuanza Julai 06

Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limetangaza kwamba mashindano ya CECAFA Kagame Cup mwaka 2024 yatafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia Julai 6 hadi 22 mwaka huu ikizishirikisha timu 16

Timu tatu alikwa, TP Mazembe (DR Congo), Nyasa Big Bullets (Malawi) na Red Arrows FC ya Zambia zote zimethibitisha ushiriki wao kujiunga na timu 13 nyingine kutoka Ukanda wa CECAFA

Awali, mashindano hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Julai 20 hadi Agosti 4 mwaka huu nchini Tanzania, lakini kutokana na ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuonyesha kuanza Agosti, CECAFA wameona mashindano yao yaanze mapema na kumalizika siku chache kabla ya kuanza kwa mtifuano wa michuano ya CAF ngazi ya klabu msimu wa 2024/2025

"Mashindano haya yatasaidia timu zetu katika ukanda huu kujiandaa vizuri kabla ya msimu wa CAF Champions League na CAF Confederation Cup 2024/2025 ambao unaanza mwezi Agosti. Kuwa na timu kubwa kutoka DR Congo, Malawi na Zambia pia kutapa msisimko kwenye mashindano yetu na kutoa changamoto halisi kwa timu zetu," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, John Auko Gecheo

Kutokana na hilo, michuano ya Cecafa Senior Challenge Cup mwaka 2024 ambayo yanahusisha timu za taifa iliyokuwa imepangwa kufungua Kalenda ya CECAFA kuanzia Juni 29 hadi Julai 14 mwaka huu, imefutwa ili kuwapa wachezaji muda zaidi wa kujiandaa na klabu zao kabla ya Cecafa Kagame Cup

Timu zitakazoshiriki michuano ya Cecafa Kagame Cup ni: Vital’O (Burundi), APR (Rwanda), El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi (Sudan), Yanga, Simba, Azam, Coastal Union (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), SC Villa (Uganda), JKU SC (Zanzibar), El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini), Nyasa Big Bullets (Malawi), TP Mazembe (DR Congo) na Red Arrows (Zambia).

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
5h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
6h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
8h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
8h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
9h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
9h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
10h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
12h ago
READ MORE →