Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetakata uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola Zambia ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Zambia katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia 2026
Bao pekee la Stars lilifungwa na Waziri Junior katika dakika ya 5 baada ya kazi nzuri kutoka Mudathir Yahya ambaye alimnyang'anya mpira kiungo wa Zambia katika eneo la hatari na kumtengenezea Waziri aliyefunga bao lake la kwanza kwa timu ya Taifa
Zambia walitawala mchezo huo kwa kutengeneza nafasi nyingi lakini uimara wa mlinda lango Ali Salim pamoja na safu ya ulinzi iliyoundwa na Mwamnyeto, Bacca, Zimbwe Jr na Mwaikenda ilikuwa kikwazo kwa Zambia
Ni ushindi ambao unaifanya Stars ifikishe alama 6 na kupanda mpaka nafasi ya pili kundi E sawa na Morocco ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili
Kwa hakika ni ushindi wa heshima kubwa kwa wachezaji wa Stars ambao walipambana kwelikweli siku ya leo