Siku ya Jumatatu, Julai 01 klabu ya Yanga inatarajiwa kuweka hadharani kikosi chake kwa ajili ya msimu wa 2024/25
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wataweka hadharani majina ya wachezaji wote waliosajiliwa na Yanga kwa ajili ya 2024/25
Hii ni pamoja na kutangaza nyota waliosajiliwa kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi msimu ujao
Aidha Yanga pia siku hiyo itatangaza ni wapi timu itakwenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya 2024/25
Likizo za wachezaji wa Yanga zinamalizika mwishoni mwa wiki ambapo kuanzia Jumatatu, Julai 01 wanatakiwa kurejea Avic Town tayari kwa mipango ya pre-season