Likizo imemalizika! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo uongozi wa Yanga umewataka wachezaji wote kuripoti Avic Town kuanzia kesho Jumatatu, Julai 08
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali kamwe amesema timu itaanza maandalizi hapo Avic Town lakini huenda baadae kikosi kitasafiri nje ya nchi
Yanga ina mualiko kutoka moja ya nchi barani Ulaya kwenda kufanya pre-season huku pia Wananchi wakiwa na mialiko kutoka nchi nyingine kwa ajili ya kwenda kucheza mechi za kirafik
Nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini ambapo Yanga itakwenda kushiriki michuano maalum itakayoandaliwa na Kaizer Chiefs
Yanga pia imealikwa nchi za Kenya na Rwanda. Baadhi ya wachezaji tayari wako jijini Dar es salaam na pengine kuanzia kesho Jumatatu wataanza kuonekana pale Avic Town



