Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto Valentine Nouma
Nouma mwenye umri wa miaka 24 anatua Simba akitokea klabu ya Fc Lupopo ya DR Congo
Nouma ambaye hucheza timu ya Taifa ya Burkina Faso anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza kushambulia akitokea eneo la ulinzi upande wa kushoto pamoja na umahiri katika ulinzi
Sifa nyingine ya Nouma ni kupiga mipira iliyokufa 'foul'
Aidha Simba pi imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kati Karaboue Chamou raia wa Ivory Coast
Karaboue ametua Msimbazi akitokea klabu ya Racing Abodjan ya huko Ivory Coast akisaini mkataba wa miaka miwili
Beki huyo mrefu ana umri wa miaka 24 tu na ndiye mrithi wa nafasi ya Hennock Inonga aliyetimkia FAR Rabat
Katika dirisha hili Simba imesajili mabeki wawili wa kati Chamou na Abdourazack Mohammed