Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini leo kuelekea Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu wa mashindano 2024/25
Simba itaondoka JNIA saa 11 jioni ambapo kikosi kitakwenda kuweka kambi ya wiki tatu katika Mji wa Ismailia
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema wachezaji wote ambao wako jijini Dar es salaam wataondoka leo lakini kuna mchezaji mmoja ambaye ataungana na timu huko Misri
"Tutaondoka Tanzania saa 11 jioni tukiwa na wachezaji wote, ni mchezaji mmoja tu ambaye ataungana nasi huko Misri," alisema Ahmed
Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davies atakuwa na wiki tatu za kukiandaa kikosi chake ambacho kimesheheni damu changa
Simba imeongeza zaidi ya wachezaji 10 wapya hivyo ni wazi Fadlu atakuwa na muda mzuri wa kujenga timu mpya kwa ajili ya kushinda makombe