Dodoma - Local - Transfer

Kipa Kagera Sugar kutua Dodoma Jiji

Joel JJ By Joel JJ
9 Jul 2024
Kipa Kagera Sugar kutua Dodoma Jiji

Dodoma Jiji iko mbioni kumsaji kipa wa Kagera Sugar raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Alain Ngeleka, ambaye alionyesha uwezo mkubwa msimu uliopita wa Ligi Kuu

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa kipa huyo aliomba kuondoka na kuvunja mkataba licha ya kwamba ulikuwa unamalizika 2025

"Hakuna shabiki yeyote wa kweli wa soka ambaye hajamuona kipa huyu. Ni kipa mzuri sana kutoka DR Congo, kusema kweli atatusaidia sana, na huu ni ushauri wa kocha wetu Mecky Mexime kwa sababu ameshaifundisha Kagera Sugar," alisema kiongozi Dodoma Jiji

Klabu hiyo pia imewaongeza mikataba wachezaji wake 10, ambao imeona wanaweza tena kuisaidia timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imeeleza wachezaji hao wataunganika na wale ambao itawasijili kwa ajili ya kuunda kikosi imara msimu ujao. Wachezaji ambao wataendelea kusalia kwa 'Walima Zabibu' hao ni Yassin Mgaza, Fadhili Mwinyimvua, Emmanuel Martin, Zidane Sereli, Augustino Nsata, Anderson Kimweri, Robison Kamura, Ntenje Albano, Apollo Onyango, na Mwana Kibuta

IPP Media

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
27m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
30m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
47m ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
50m ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →