Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Julai 16 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jul 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Julai 16 2024

Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe ni mmoja wa makocha wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Gareth Southgate iwapo ataamua kujiuzulu kama kocha wa timu ya taifa ya England

Wachezaji wa zamani wa England Steven Gerrard na Frank Lampard pia wanatazamiwa kuwania nafasi hiyo. (Guardian)

Manchester United wamemuulizia beki wa Ujerumani Jonathan Tah huku Bayern Munich wakishindwa kufikia makubaliano na Bayer Leverkusen kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Florian Plettenberg)

Arsenal wamekataa ofa ya Fulham ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 23. (Standard)

Liverpool na Atletico Madrid wanavutiwa na mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Mohamed Simakan mwenye umri wa miaka 24. (Sky Germany)

Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 31, anatazamiwa kujiunga na AC Milan kwa mkataba wa miaka minne kutoka Atletico Madrid. (Fabrizio Romano)

Manchester City wamepiga hatua katika juhudi za kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26, kutoka RB Leipzig. (Football Insider)

Bayern Munich pia wanavutiwa na Olmo, ambaye alifunga mabao matatu wakati wa Euro 2024 alipoisaidia nchi yake kushinda michuano hiyo. (Fabrizio Romano)

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Mikel Merino ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na Barcelona kuimarisha safu yao ya kati, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa Real Sociedad. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Arsenal pia wanapania kumnunua Merino, ambaye aliwahi kuichezea Newcastle United kabla ya kurejea Uhispania. (Telegraph - usajili unahitajika) Newcastle United iko tayari kumenyana na Everton katika harakati za kumsajili winga wa Italia Wilfried Gnonto mwenye umri wa miaka 20 kutoka klabu ya Leeds United. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 35, anakaribia kujiunga na klabu ya Saudi Arabia ya Al-Qadsiah. (Sky Sports)

Southampton wamekubali dili la hadi £18m kumsajili kiungo wa kati wa England Flynn Downes, 25, kutoka West Ham. (Standard - usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’