Yanga hiyooo Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th July 2024


Yanga hiyooo Afrika Kusini

Alhamisi ya wiki hii Yanga inatarajiwa kusafiri Afrika Kusini kushiriki michuano maalum Mpumalanga Premier’s International Cup

Michuano hiyo imedhaminiwa na Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC) kwa kushirikiana na TS Galaxy Foundation

Ni michuano maalum ya pre-season ambayo pamoja na Yanga, timu nyingine zitakazoshiriki ni TS Galaxy Fc, Mbabane Swallows Fc na Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

Augsburg ilianzishwa mwaka 1907, ni klabu kubwa zaidi ya soka katika Swabian Bavaria yenye wanachama 25,000, ilipanda daraja Bundesliga kwa mara ya kwanza mwaka 2011, ambako imebaki tangu wakati huo. Katika msimu wa 2015/16, ilicheza Ligi ya Europa kwa mara ya kwanza

Augsburg itachuana na Yanga katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utakaopigwa Jumamosi, Julai 20, Mbombela Stadium moja ya viwanja vilivyotumika katika michuano ya kombe la Dunia mwaka 2010

SABC watarusha mechi hiyo mbashara pamoja na mechi nyingine zitakazofuata

Baada ya mchezo huo, Wananchi wataendelea kusalia Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumapili, Julai 28


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.