Kiungo wa KMC Awesu Awesu yuko mbioni kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba, imefahamika
Simba na KMC tayari zimefikia makubaliano na kiungo huyo aliyekuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na watoza ushuru hao wa Kinondoni
Wiki iliyopita Awesu aliandika barua ya kuomba kuvunja mkataba huo lakini mabosi wa KMC wakamuwekea ngumu wakimtaka awasilishe mezani ofa ya timu inayomuhitaji
Awesu anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kisha kusafiri Misri kuungana na kikosi cha Simba kinachoendelea na pre-season
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametamba kuwa watafunga dirisha la usajili kibabe kwa kushusha mashine za 'UBAYA UBWELA'