Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Julai 17 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Jul 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Julai 17 2024

Real Madrid wanavutiwa na beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad kumuuza Moussa Diaby, Marseille wakubali dili la kumnunua Mason Greenwood wa Manchester United. Real Madrid wana hamu ya kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 25, ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Liverpool. (Talksport)

Manchester United hawana nia ya kumnunua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate endapo wataamua kumfuta na Erik ten Hag. Badala yake, mkufunzi wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel anaonekana kupendelewa zaidi. (Mail)

Newcastle United wamesema watapambana kumbakisha mkufunzi wao Eddie Howe baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kuhusishwa na tetesi za kuchukua nafasi ya Gareth Southgate aliyejiuzulu kama kocha wa Uingereza. (Guardian)

Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad ikiwa klabu hiyo ya Ligi ya Saudi Pro inataka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Diaby, 25. (Sportsport)

Manchester United wanajadiliana kuhusu masuala ya kibinafsi na wawakilishi wa mlinzi wa Ufaransa Leny Yoro baada ya kupokea ofa ya pauni milioni 52 iliyokubaliwa na Lille kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Yoro pia ananyatiwa na Real Madrid. (Guardian)

Marseille wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood, 22. (The Athletic - usajili unahitajika)

Aston Villa inajiandaa kumenyana na Chelsea na Barcelona kumsajili winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22 ambaye aliichezea Uhispania katika michuano ya Euro 2024. (Teamtalk)

Al-Nassr wamekamilisha mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango wa Manchester City Ederson, 30, baada ya ofa yao ya euro 30m kukataliwa. Klabu hiyi ya Saudia sasa inajaribu kumsajili mchezaji mwenzake wa Brazil Bento, 25, anayechezea Athletico Paranaense. (Fabrizio Romano)

Arsenal wanatarajia kupokea ofa zaidi kwa kiungo Emile Smith Rowe, 23, baada ya kukataa ombi la Fulham la kumsajili Muingereza huyo, huku Crystal Palace pia wakimtaka. (Evening Standard)

Cole Palmer amejaribu kumshawishi mchezaji mwenzake wa England na mshambuliaji wa Aston Villa Ollie Watkins, 28, kujiunga na Chelsea msimu huu wa joto. (Football Insider)

Leicester City wamewasilisha ofa ya pauni milioni 21m na na nyongeza ya oauni milioni nne kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Argentina Matias Soule, 21, lakini Juventus, wanataka pauni milioni 25 kumuachia mchezaji huyo. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’