Yanga - Simba - Azam - Local

Serikali yapongeza VAR kutumika Ligi Kuu Tanzania Bara

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Jul 2024
Serikali yapongeza VAR kutumika Ligi Kuu Tanzania Bara

Serikali imesema kupatikana VAR ambayo itatumika kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, kutapunguza malalamiko waliyokuwa wanatupiwa waamuzi kwa kile kilichokuwa kinaonekana hawafanyi maamuzi sahihi

Akizungumza jana kwenye hafla ya uzinduzi wa video ya usaidizi wa waamuzi maarufu kama VAR, uliofanyika kwenye Uwanja wa Banjamin Mkapa, Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alisema kuwapo kwa kifaa hicho kitawezesha waamuzi kufanya maamuzi yao sahihi kwani watakuwa na uwezo wa kurudia kile ambacho watakuwa hawajakiona, ili timu ziweze kupata ushindi wa halali

Aidha, Waziri Majaliwa, alitaka viwanja ambavyo havina ubora, viwekwe pembeni kwani kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu, vitaharibu mvuto wa ligi yenyewe

"Nampongeza Rais Karia (Wallace) kwa juhudi kubwa tangu aanze kulisimamia Shirikisho la Mpira wa Miguu tumepata mafanikio makubwa kupitia mpira wa miguu, na kwa maboresho haya naamini Tanzania itapanda na kushika nafasi ya nne kwenye Ligi ya Afrika kutokana na uwekezaji huu," alisema Waziri Mkuu

Alisema serikali inalitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuendelea kushirikiana na kampuni zilizowekeza kwenye utangazaji wa michezo mbalimbali nje na ndani ya nchi, ili kukuza soka la nchi na kulitangaza nje, pamoja na kuwaweka sokoni wachezaji wa Kitanzania.

Nae Rais wa TFF, Karia, alisema kuwa wameamua kubaki na idadi ya wachezaji 12 wa kigeni licha ya wadau wengi kutaka idadi hiyo ipunguzwe

Alisema sababu kuwa ni kwamba klabu za Tanzania zimepata mafanikio makubwa kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwa na wachezaji wa kigeni, ambapo kabla ya hapo zilikuwa hazifanyi vema

"Kwa takwimu tulizonazo wachezaji wa kigeni hawajafika 70 kati ya wachezaji 600 ambao huwa wanashiriki Ligi Kuu, hivyo wachezaji wetu wanatakiwa na wao watoke nje ili wakapate changamoto na siyo sisi kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni," alisema Rais Karia

Alisema wachezaji wa kigeni wameongeza ushindani kwenye Ligi Kuu na kuchangia kukua kwa viwango vya wachezaji wa ndani, kiasi cha kuisaidia timu ya taifa kufanya vizuri

"Tulipokuwa tukicheza na DR Congo na Zambia, wachezaji wengi wa Tanzania walikuwa wa ligi ya ndani na wadogo, lakini walifanya vizuri sana kiasi cha kushangaza wengi, kwa sababu hawana tena ule woga wa kuogopa wachezaji wa kigeni, kila siku wanacheza na wachezaji hao hao kwenye ligi au wapo timu moja, hiyo imetusaidia sana kama taifa," alisema

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’