Kocha Simba afurahia ushindi wa kwanza Misri

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jul 2024
Kocha Simba afurahia ushindi wa kwanza Misri

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Qanah katika mchezo wa kwanza wa kirafiki ambao Simba ilicheza jana Misri, Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davies ameeleza kuridhishwa kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo huo

Fadlu amesema kile alichokifanyia kazi katika kipindi cha wiki mbili za pre-season huko Misri kimeanza kuonekana lakini huo ni mwanzo tu

"Nafurahi tumeweza kushinda mechi kwa mabao 3-0 lakini muhimu wachezaji wamecheza vizuri, baada ya wiki mbili za mazoezi, hii ni hatua nzuri kwetu"

"Hii ni mechi maalum ya kimkakati zaidi, tulianza vyema na kufunga mabao mawili katika kipind cha kwanza kama tusingefanya mabadiliko ya wachezaji tulikuwa na nafasi ya kufunga hata mabao matano"

"Ilikuwa mechi ambayo tulilenga kumpa nafasi kila mchezaji ili tuone ni kwa namna gani tumefanikiwa katika maandalizi yetu. Kila mchezaji alipata angalau dakika 30 za kucheza ni wachezaji wawili tu (Awesu na Onana) ambao walichelewa kuungana nasi hapa Misri hivyo walicheza kwa dakika 20"

"Baadhi ya wachezaji tuliwapa muda zaidi (dakika 60) kwa kuzingatia utimamu na utayari wao baada ya muda huu mfupi wa mazoezi"

"Lakini nisema bado tuna kazi ya kufanya, kwa wastani tulihitaji angalau wiki sita za maandalizi. Tuna timu mpya wachezaji wengi hapa ni wageni, tunahitaji kuwajenga kimbinu pamoja na kupata mechi zaidi za kirafiki"

"Mpaka kufikia Simba Day tutakuwa tumepata angalau wiki nne, bila shaka tutakuwa katika hatua nzuri zaidi na baada ya muda mfupi tutafikia malengo na matarajio yetu ya kuwa na timu bora na ya ushindani," alisema Fadlu

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
31m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’