Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Julai 27 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jul 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Julai 27 2024

Miamba ya soka la England klabu ya Manchester City inapanga kumfanya kiungo wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Jamal Musiala, 21, kuwa mrithi wa kiungo mchezeshaji wao Kevin de Bruyne, 33. (CaughtOffside)

Barcelona wamefikia makubaliano ya kumsajili winga wa klabu ya Athletic Bilbao na timu ya taifa ya Uhispania Nico Williams, 22, kwa mkataba wa miaka mitano, ambao pia utakuwa na kipengele cha nyongeza ya mwaka mmoja. (Nicolo Schira)

Tottenham ipo mbele ya Liverpool na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Federico Chiesa, 26. (Football Transfers)

Klabu ya Arsenal inataka kulipwa dau la walau euro milioni 50 (pauni 42m) ili kumuuza mshambuliaji wao raia wa Uingereza Eddie Nketiah, 25, ambaye mpaka sasa ameivutia klabu ya Ufaransa ya Marseille. (La Provence - in French)

Newcastle United wana imani kuwa winga wao Anthony Gordon atasalia kwenye klabu hiyo licha ya kufuatiliwa na Liverpool. (Team Talk)

West Ham wanajipanga kuongeza dau ili kumnasa mshambuliaji Jhon Duran, 20, kutoka Colombia ambaye klabu yake ya sasa Aston Villa inataka pauni milioni 40 ili kumuachia. (Standard)

Manchester United wamerejea katika mbio za kutaka kumsajili beki wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Morocco Noussair Mazraoui, 26, baada ya mipango yake ya kuhamia West Ham kushindikana. (Sky Germany)

Mazraoui anatazamiwa kutaka kuhakikishiwa kuwa atapata muda wa kutosha wa kucheza kabla ya kukubali kujiunga na United. (Manchester Evening News)

Tottenham wapo kwenye mazungumzo na klabu ya Girona ili kuwauzia mshambuliaji wao raia wa Uhispania Bryan Gil, 23, ambaye tayari ameshaafikiana na Girona kuhusu maslahi yake binafsi. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kubadilishana beki wao Aaron Wan-Bissaka, 26, na Denzel Dumfries, 28, kutoka Inter Milan. (Telegraph - subscription required)

Chelsea wanajiandaa kuwaruhusu wachezaji 12 kuondoka katika klabu hiyo kwenye dirisha hili la usajili baada ya mkataba wa beki wao raia wa Ufaransa Malang Sarr, 25, kuvunjwa ili kumuwezesha kujiunga na klabu ya RC Lens. (Sun)

Los Angeles FC wamepiga hatua katika mazungumzo yao kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann, 33. (L'Equipe - in French)

Klabu hiyo inayocheza ligi ya Marekani (MLS) pia wapo karibu kumsajili kwa mkopo kiungo raia wa Uingereza Lewis O'Brien, 25, kutoka katika klabu ya Nottingham Forest. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’