Yanga imebeba Toyota Cup ugenini ikiifumua Kaizer Chiefs mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Toyota Bloemfontein huko Afrika Kusini
Unaweza kusema ilikuwa mechi ya Yanga kudhihirisha umwamba mbele ya kocha wake wa zamani Nasreddine Nabi ambaye vijana wake walikuwa na wakati mgumu
Alikuwa ni Prince Dube aliyefungua kalamu ya mabao akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Chiefs kabla ya Aziz Ki kuongeza la pili akipokea pasi ya Duke Abuya
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 na ikarejea kipindi cha pili kuongeza mengine mawili kupitia kwa Aziz Ki na Clement Mzize
Aziz Ki alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki takribani 46,000
Hii ilikuwa mechi inayohitimisha pre-season ya Yanga Afrika Kusini ambapo sasa Wananchi wanarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya wiki ya Mwananchi



