Yanga - Simba - Azam - Local

Kanuni Ligi Kuu 2024/25 zimeboreshwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Aug 2024
Kanuni Ligi Kuu 2024/25 zimeboreshwa

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha kanuni 12 mpya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajili ya msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza hivi karibuni

Taarifa iliyotolewa na TFF jana, ilisema kuwa, kamati hiyo ilipitisha kanuni hizo, Agosti Mosi, baada ya kujadili na kufanyia kazi maoni ya wadau mbalimbali wa soka kwa ajili ya kanuni mpya za ligi

Taarifa imesema kuwa kanuni zilizofanyiwa maboresho na kupitishwa katika kikao hicho ni pamoja na kanuni ya saba ya 'firts league' kuhusu nane bora, kanuni ya tisa ya ligi kuhusu uwanja, kanuni ya 17 kuhusu taratibu za mchezo, kanuni ya 31 kuhusu timu kutofika uwanjani, kanuni ya 47 kuhusu udhibiti wa klabu, kanuni ya 62 kuhusu wachezaji wa kigeni, kanuni ya 77 kuhusu makocha na kanuni ya 79 kuhusu maamuzi yasiyokatiwa rufaa

Baadhi ya kanuni mpya ni ya ushirikina uwanjani, ambapo sasa badala ya fainli ya Sh. 500,000, mpaka Sh. Milioni Moja, sasa timu zitakazobainika kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina, zitatozwa faini ya chini kuanzia Sh. Milioni Tano hadi Milioni10, lakini kama hali hiyo ikionekana inajirudia, klabu itapigwa faini ya Sh. Milioni 20

Kanuni nyingine ni ya ada ya usajili wa wachezaji kutoka nje ya nchi, ambapo sasa klabu zitalazimika kulipa Sh. Milioni Nane, ambapo klabu zenye wachezaji wote 12 wanaoruhiwa kikanuni, zitalazimika kujikamua Sh Milioni 96

Pia ipo kanuni ya kuwapiga marufuku wachezaji na viongozi kujihusisha na michezo ya kubashiri, yaani 'kubeti', huku ikiwepo kanuni kwamba kila mchezo lazima wawepo wachezaji wawili kutoka timu ya vijana, ambao watakuwa wameorodheshwa kwenye orodha ya wachezaji waliovaa jezi

Pia ipo kanuni inayowataka makocha wote wakuu wa kigeni nje ya Afrika wawe angalau wana cheti cha ukocha cha 'Pro Diploma', na wasaidizi wa kigeni nje ya Afrika wanatakiwa kuwa na elimu ya 'Diploma A.'

IPP Media

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
33m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’