Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu August 19, 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Aug 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu August 19, 2024

Wawakilishi wa mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney wako kwenye mazungumzo na klabu ya Saudi Pro League Al-Ahli ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Teamtalks)

Manchester United hawana nia ya kutaka kumnunua Toney. (Sky Germany). Manchester City wanataka meneja Pep Guardiola, 53, kuamua iwapo atasaini mkataba mpya na klabu hiyo kabla ya Krismasi. Mkataba wa sasa wa Mhispania huyo utaendelea hadi 2025. (Sky Sports)

Nottingham Forest, Villarreal, Sevilla, na Valencia wanataka kumnunua beki wa Aston Villa na Uhispania Alex Moreno, 31. (Football Insider)

Panathinaikos iko kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu mkataba wa kiungo wa kati wa Uruguay Facundo Pellistri, 22. (Athletic – Subscription Required)

Atletico Madrid hawajapuuza uhamisho wa kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Javi Guerra mwenye umri wa miaka 21 huku mkataba wao wa kiungo wa kati wa Chelsea na Muingereza Conor Gallagher, 24, ukikwama. (Subscription Required)

Liverpool itasubiri hadi dirisha la usajili la Januari kumsajili kiungo nyota baada ya hatua ya klabu hiyo kumnunua Mhispania Martin Zubimendi, 25, kutoka Real Sociedad kushindikana. (Football Insider)

Fulham wameanzisha tena mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 27. (Sky Sports)

Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Giovanni Manna amekataa kufuta mpango wa kumnunua McTominay. (Manchester Evening News)

Klabu hiyo ya Serie A pia imekubali mkataba wa kumsajili winga wa Brazil David Neres, 27 kutoka Benfica. (Fabrizio Romano)

Las Palmas wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Fulham raia wa Brazil Carlos Vinicius, 29, ambaye pia anasakwa na Corinthians. (Sky Sports)

Crystal Palace wamefanikiwa katika kumsaka beki Mfaransa Maxence Lacroix, 24, kutoka Wolfsburg. (Sky Germany)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’