Azam - Local

Dabo ataja sababu ya ushindi mwembamba nyumbani CAF CL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Aug 2024
Dabo ataja sababu ya ushindi mwembamba nyumbani CAF CL

Kocha wa Azam Fc, Youssouph Dabo, amesema hawakupata ushindi mkubwa nyumbani kwa sababu wachezaji wake walionekana kucheza kwa presha ya kutaka kufunga mabao mapema na walipokuwa wanashindwa kufanya hivyo walikuwa wanatoka mchezoni na kushindwa kufuata maelekezo yake

Raia huyo wa Senegal, alisema hayo baada ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya APR ya Rwanda kwenye mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam juzi

Pamoja na ushindi huo kiduchu, kocha huyo alisema ana matumaini ya timu yake kusonga mbele na kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo

"Nafikiri wachezaji walikuwa na hofu, kama walikuwa wanataka kufunga mabao ya haraka haraka dakika za mwanzo, lakini kila muda ulivyozidi kwenda hawapati, walikuwa wakiingiwa na presha na kushindwa kucheza kwa maelekezo"

Mapumziko niliwaambia wasiwe na haraka kwa sababu hii ni mechi ya kwanza, ya marudiano tutacheza Rwanda, hivyo watulie, watapata nafasi watafunga na hata wasipofanya hivyo leo (juzi), hata mechi ya mkondo wa pili wanaweza kufunga pia," alisema Dabo

Azam ilipata ushindi huo kwa bao lililofungwa na straika raia wa Colombia, Jhonier Blanco dakika ya 56 kwa mkwaju wa penalti, baada ya Feisal Salum kuangushwa ndani ya eneo la hatari

"Nimeifutilia APR ni timu ambayo huwa hairuhusu mabao kirahisi, mabeki wake wapo vizuri, kwa maana hiyo inabidi tujipange vema katika mechi ya marudiano"

"Tunakwenda kucheza nchini Rwanda, tuna uhakika wa kushinda kwa sababu tuna kikosi kizuri cha kuweza kushinda pia ugenini," alisema kocha huyo

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’