Freddy kuibukia USM Alger

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st August 2024


Freddy kuibukia USM Alger

Wakati mshambuliaji Leonel Ateba akitua Msimbazi akitokea klabu ya USM Alger, Freddy Michael aliyempisha Mcameroon huyo nae ameelekea USM Alger

Lakini haukuwa usajili wa kubadilishana wachezaji, Simba imetumia zaidi ya Milioni 540 kumn'goa Ateba huku ikifikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba wa Freddy ambaye hakukidhi mahitaji ya kocha Fadlu Davies

Tayari Freddy ameondoka nchini kuelekea Algeria kujiunga na USM Alger, mabingwa wa zamani wa kombe la Shirikisho Afrika CAF CC

Freddy atakuwa mchezaji wa tatu kucheza ligi kuu ya Algeria msimu huu akitokea klabu ya Simba

Wachezaji wengine ni Sadio Kanoute na Babacar Sarr waliojiunga na JS Kabylie inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba Abdelhak Benchikha


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.