Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 12 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Sep 2024
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 12 2024

Newcastle wanamfanya Angel Gomes kuwa mlengwa wao mkuu, Galatasaray wanajiandaa kutoa ofa kwa Emerson Palmieri, Wesley Fofana anafikiriakuihama Chelsea na kujiunga na Marseille msimu huu wa joto

Kiungo wa kati wa Uingereza na Lille Angel Gomes amekuwa akitajwa kuwa ni mlengwa mkuu wa Newcastle , lakini Liverpool , Tottenham na Borussia Dortmund pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.(Sun)

West Ham wanajiandaa kupokea ofa kutoka kwa Galatasaray kwa ajili ya beki wa Italia Emerson Palmieri, 30. (Football Insider)

Beki Mfaransa Wesley Fofana, 23, anasema alifikiria kuondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya nyumbani ya Marseille msimu huu wa joto. (Free Foot - kwa Kifaransa)

Manchester City , Chelsea na Liverpool wanavutiwa na kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Chris Rigg, 17. (Givemesport)

Mauricio Pochettino, 52, atapokea mshahara wa kila mwaka wa karibu $6m (£4.6m) kama meneja wa Marekani . (ESPN)

Shirikisho la soka England limezungumza na baadhi ya wasimamizi wengine licha ya kipindi cha faraja cha Lee Carsley hadi sasa kama kocha wa muda wa England. (Telegraph - usajili unahitajika)

Meneja wa zamani wa England Gareth Southgate, 54, anasema kazi yake inayofuata inaweza kuwa tofauti na soka. (Sky News)

Fifa iko kwenye mazungumzo ya kupanua Kombe la Dunia la Wanawake hadi timu 48 mapema kufikia 2031, kulingana na ukubwa wa mashindano ya wanaume. (Telegraph - usajili unahitajika)

Tottenham , Newcastle na Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 24, ingawa Juventus pia wanavutiwa naye. (TuttoJuve)

Chelsea na Tottenham bado wanavutiwa na mlinzi wa Lecce wa Denmark Patrick Dorgu, 19, ambaye thamani yake ni takriban euro 40m (£33.8m). (La Gazzetta dello Sport kupitia SportWitness)

Mlinzi wa Monaco na Brazil Vanderson, 23, ameivutia sana Chelsea , huku Manchester United na Tottenham pia wakimtaka nyota huyo(Caughtoffside)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’