Yanga - Simba - Azam - Singida - Local

Morocco ataja siri ya ushindi wa Stars Ivory Coast

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Sep 2024
Morocco ataja siri ya ushindi wa Stars Ivory Coast

Kocha wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars', Hemed Morocco, amesema kujituma kwa wachezaji na kufuata maelekezo yake muda wote wa mchezo ndio sababu ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya Guinea juzi usiku

Stars ikiwa ugenini juzi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 'kusisimua' wa mabao 2-1 na kuendelea kuweka hai na kukoleza mbio za kushiriki fainali za AFCON mwakani nchini Morocco.

Ushindi huo pia umepongezwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo kupitia ukurasa wake wa kijamii alisema;

"Hongera kwa vijana wetu wa Taifa Stars kwa ushindi mlioupata dhidi ya Guinea katika mchezo mlioucheza hapo jana (juzi)", alisema Rais Samia

Aidha, Rais Samia ameitakia mafanikio mema Taifa Stars katika michezo mingine iliyopo mbele yao ya kuwania kufuzu Fainali hizo za AFCON

Stars juzi iliingia kwenye mchezo huo huku ikiwa imetoka kubanwa mbavu nyumbani na Ethiopia waliowalazimisha kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa

Morocco amesema matokeo ya mchezo wao dhidi ya Ethiopia hayakuwafurahisha lakini yaliwaongezea morali ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa juzi

"Baada ya mchezo na Ethiopia tulirudi kwenye uwanja wa mazoezi na kuanza kuyafanyia kazi mapungufu tuliyoyaona, lakini lazima niwapongeze wachezaji wangu kwa hali yao ya kujituma na kufuata maelekezo yote, hii ndio imepelekea tumepata ushindi huu muhimu," alisema Morocco

Alisema matokeo kwenye mchezo dhidi ya Ethiopia yaliwaumiza sana lakini wachezaji wake wameonyesha ukomavu mkubwa kwa kupambana dakika zote 90 kwenye mchezo wa juzi

"Japo niliamini kama tutapambana muda wote tunaweza kupata ushindi, sikutegemea wachezaji kujituma namna ile na kufuata maelekezo yangu kwa asilimia kubwa, ushindi huu umechochea morali kuelekea michezo inayofuata," alisema kocha huyo.

Magoli kwenye mchezo wa juzi yalifungwa na nyota wa Azam FC, Feisal Salum 'Feitoto' aliyefunga bao la kusawazisha baada ya awali Stars kutanguliwa kwa bao moja, goli la pili na la ushindi lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mudathir Yahaya

Matokeo hayo yameifanya Taifa Stars kushika nafasi ya pili kwenye kundi H wakiwa na pointi nne, pointi mbili nyuma ya vinara Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku Ethiopia wakishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi moja na Guinea wanaburuza mkia kwa kutokuwa na pointi huku kila timu ikiwa imecheza michezo miwili

IPP Media

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’