Coastal - Local

Coastal Union yakana kumrejesha Mgunda

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Sep 2024
Coastal Union yakana kumrejesha Mgunda

Klabu ya Coastal Union imekana kutaka kumrudisha kocha wake wa zamani, Juma Mgunda ili kukinoa kikosi hicho

Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Abbas El Sabri, amesema taarifa za Mgunda kutaka kurejea Coastal Union si za kweli, lakini akakiri kuwa viongozi wapo kwenye mchakato wa kusaka Kocha Mkuu na watu wa benchi la ufundi

Sabri alisema Coastal imelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na taarifa nyingi ambazo zinaihusisha timu hiyo na Mgunda, ambaye amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Simba

"Hakuna taarifa yoyote juu ya Juma Mgunda kwenye klabu yetu, tunajua yeye alikuwa mchezaji wetu zamani na alihudumu kwa mafanikio makubwa, pia alikuwa kocha na kufanya mambo makubwa"

"Kusema hatumuhitaji ni kumkosea heshima, lakini kwa sasa hakuna mipango hiyo ya kuzungumza naye, badala yake uongozi bado unaendelea na mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu na watu wa benchi la ufundi, lakini siyo Mgunda, timu iko chini ya Kocha Joseph Lazaro ambaye anakaimu na amekuwa akifanya vizuri na viongozi wameonyesha kuwa na imani naye," alisema El Sabri

Tetesi zinasema kuwa klabu zilizokuwa zikimtolea macho Mgunda ni Coastal na Namungo. Kabla ya kutua Simba, Mgunda alikuwa kocha wa Coastal na alichukuliwa kuziba nafasi ya Zoran Maki ambaye aliondoka mapema kwenye klabu hiyo kabla ligi wala michezo ya kimataifa haijaanza, aliiwezesha kutinga hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika

IPP Media

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
30m ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
4h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
5h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
7h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’