Azam Fc wameendeleza mwanzo mbaya wa msimu huu 2024/25 baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Pamba Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex
Huo ni mchezo wa pili mfululizo kwa Azam Fc wanakosa ushindi wakiambulia alama moja
Pamba almanusra waondoke na alama zote tatu kama sio mwamuzi Tatu Malogo kulikata bao hilo na kuamuru mpira wa adhabu kuelekea Azam Fc kwani kabla ya bao hilo kufungwa mshambuliaji George Mpole alifanyiwa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari
Azam Fc ilifanya mabadiliko ya benchi la ufundi ambapo Rachid Taoussi raia wa Morocco jana aliiongoza timu hiyo katika mechi ya kwanza akichukua nafasi ya Yusuf Dabo
Hata hivyo ni wazi Taoussi ana kazi ya kufanya kurejesha makali ya Azam Fc kabla ya kukutana na Simba katika mchezo unaofuata Septemba 26