Simba - Local

Al Ahli Tripoli waifanyia vurugu Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2024
Al Ahli Tripoli waifanyia vurugu Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao iko salama licha ya 'purukushani' zilizojitokeza uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Tripoli uliopigwa jana huko Libya

Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, mashabiki wa Al Ahly Tripoli walifanya vurugu uwanjani kwa kuwarushia chupa wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi

Ahmed amesema timu ililazimika kukaa uwanjani kwa takribani dakika 40 kabla ya kupanda basi kuelekea hotelini

"Tunashukuru tuko salama pamoja na vurugu zilizojitokeza, tumerejea hotelini salama kabisa"

"Baada ya mchezo kumalizika vurugu zilijitokeza uwanjani, maafisa usalama walitushauri tuende vyumbani tusubiri mashabiki waondoke uwanjani ndipo nasi tuondoke"

"Hivyo tulikaa uwanjani kama dakika 40 ndipo tukapanda basi kuelekea hotelini. Kulikuwa na tukio la golikipa wetu Aishi Manula kushambuliwa wakati tunatoka jukwaani kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo, lakini tunashukuru nae hakupata madhara yoyote"

"Manula alishambuliwa na moja ya maafisa wa usalama katika tukio la kushangaza kwani ni wao waliotushauri tuende katika vyumba vya kubadilishia nguo tusubiri vurugu zutulie," alisema Ahmed

Simba inatarajiwa kuondoka leo kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili ijayo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’