Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 16 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 16 2024

Newcastle wanamfuatilia winga wa Bayern Munich Mjerumani Leroy Sane, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)

Bayern Munich pia wanazidisha mazungumzo na Jamal Musiala, 21, kuhusu kuongeza mkataba, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Ujerumani ukikamilika 2026. (Sport1 – In Detsch)

AC Milan, Inter Milan na Napoli wote wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Torino mwenye umri wa miaka 23 Samuele Ricci. (Calciomercato – In Italy)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl ametetea kuuzwa kwa mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 25, kwa Manchester United, akisema mabeki wa kati wa sasa wa klabu hiyo wana uwezo zaidi wa kuweka ulinzi juu zaidi ya uwanja. (Mirror)

Mfanyabiashara wa Marekani John Textor anamtaka nyota wa muziki Jay-Z kushirikiana naye katika kuinunua Everton. (Sun)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 29, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Sky Sports Germany)

Kimmich, hata hivyo, ananyatiwa na Barcelona anapokaribia mwisho wa mkataba wake wa sasa na klabu hiyo ya Bundesliga. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Liverpool haiwezi kumnunua beki wa kati wa Sevilla Loic Bade, 24, licha ya kuhusishwa na Mfaransa huyo. (Matteo Moretto, via Yahoo)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Jamaica Michail Antonio, 34, na mshambuliaji wa Uingereza Danny Ings, 32, wote wanaweza kuondoka West Ham kabla ya kukamilika kwa mikataba yao msimu ujao. (Football Insider)

Barcelona wanasema wanataka kumbakisha fowadi wa Uhispania Ansu Fati licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoichezea klabu hiyo mchezo wowote wa ligi tangu Agosti 2023, kabla ya kutolewa kwa mkopo kwa Brighton msimu uliopita . (Fabrizio Romano)

Manchester United walizuiliwa katika mbinu zao za kumsajili beki wa Senegal Mikayil Faye, 20 kabla ya kujiunga na Rennes kutoka Barcelona. (Inkubator podcast, via Teamtalk)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’