Mashujaa - Local - Yanga

Ngushi apania kurejesha makali Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2024
Ngushi apania kurejesha makali Ligi Kuu

Mshambuliaji Crispin Ngushi, amefunga bao lake la pili kwenye Ligi Kuu Tanzania, likiwa pekee katika mchezo ambao timu yake ya Mashujaa FC ilishinda 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam akisema lengo lake ni kufika mbali zaidi, hata kama itakuwa ni kurejea kwenye klabu yake ya zamani, Yanga

Ngushi, ambaye alijiunga na Mashujaa kwa mkataba wa mwaka mmoja, akitokea timu hiyo aliyoifunga Ijumaa iliyopita, Coastal Union ambako alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka Yanga, alisema anashukuru kwa kupachika bao katika mchezo huo ambalo limekuwa la pili katika michezo mitatu tu aliyocheza akiahidi makubwa zaidi msimu huu

"Siri ni kwamba Mashujaa ninachokipata naridhika nacho, hata Yanga ilikuwa hivyo ila nilikuwa sipati sana muda wa kucheza kama huku, nitazidi kufanya mazoezi kwa bidii ili niweze kufunga zaidi, hata ikitokea timu yoyote kubwa inanitaka, au kurudi Yanga nitashukuru Mungu kwa sababu lengo langu ni kucheza mpira ili niweze kufika mbali," alisema straika huyo

Alipoulizwa kama kwa moto huo aliouwasha ameingia kwenye kinyang'anyiro cha ufungaji bora, alijibu ni mapema mno kwa sasa kuongelea hilo

"Kuhusu ufungaji bora, hayo ni mambo ya mbele sana, ila kwa sasa wacha nipambane, kila mechi kwangu ni fainali," alisema

Kabla ya bao hilo, Agosti 17, mwaka huu alifunga bao moja lililoipa ushindi wa 1-0, Mashujaa FC dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, likiwa ni bao la kwanza kufungwa msimu huu wa ligi 2024/25

Straika huyo alisajiliwa 2022 na Yanga kutoka Mbeya Kwanza, lakini baada ya kukosa namba, klabu hiyo ilimpeleka Coastal Union kwa mkopo wa mwaka mmoja, ambapo aliumaliza mwishoni mwa msimu uliopita na msimu huu amesajiliwa Mashujaa kama mchezaji huru

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’