Simba - Local

Kocha Simba afurahia suluhu Libya

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2024
Kocha Simba afurahia suluhu Libya

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amewapongeza wachezaji wake kwa nidhamu waliyoionyesha katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli

Mchezo huo uliopigwa dimba la Tripoli International jana, ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, Simba ikifanikiwa kuondoka na 'cleensheet' ugenini

"Nawapongeza wachezaji wangu kwa nidhamu ya mchezo walioonyesha leo. Tumedhihirisha kwa kiasi gani tunaweza kuwa bora tukicheza bila ya mpira"

"Tulitengeneza nafasi kubwa za kufunga katika kipindi cha kwanza, mechi kubwa za aina hii hupati nafasi nyingi hivyo ni muhimu kutumia nafasi chache zinazopatikana, bahati haikuwa upande wetu"

"Ilikuwa ni mechi ya kimkakati zaidi ambayo naona tumefanikiwa kwani hatukuruhusu bao ugenini"

"Mashabiki wa Al Ahly Tripoli walifanya mazingira ya mchezo huu kuwa magumu, nawapongeza kwa kujaza uwanja lakini naamini mashabiki wa Simba watafanya zaidi"

"Waje kwa wingi watuunge mkono katika mchezo wa marudiano, tuna nafasi ya kumaliza mchezo huu nyumbani," alisema fadlu

Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote katika uwanja wa Benjamin Mkapa ili kutinga hatua ya makundi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’