Kikosi cha Simba kimerejea salama jijini Dar es salaam Alfajiri ya leo Jumatano, wkitokea Libya ambako walikamilisha mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli
Baada ya kutua, Wekundu hao wa Msimbazi wameeleka kambini Mbweni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili, Septemba 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa







