Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Septemba 19 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Septemba 19 2024

Chelsea wako tayari kumruhusu winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, huku klabu ya Ufaransa ya Marseille ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (TeamTalks)

Arsenal wameanza mazungumzo ya kandarasi na beki wa kati Gabriel Magalhaes, 26, ingawa mazungumzo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil yako katika hatua za awali. (Football Insider)

Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen alihusishwa na kuondoka Manchester United msimu uliopita, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, anasema hakufikiria kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Mail)

Mshauri wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic amewasiliana na meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic, huku meneja wa timu hiyo ya Serie A Paulo Fonseca - ambaye aliteuliwa msimu wa joto - tayari akiwa chini ya shinikizo baada ya kuanza vibaya msimu. (Sky Sports Ujerumani)

Rais wa Inter Milan Guiseppe Marotta anasema klabu hiyo ilikuwa karibu kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 24, alipokuwa na umri wa miaka 15, kabla ya mpango wa uhamisho huo kuharibika (Soka Italia)

Beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell bado anatarajiwa kuondoka Chelsea mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kurejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza baada ya kushindwa kupata uhamisho msimu wa joto. (Football Insider)

Chelsea inaweza kumteua Sachin Gupta, ambaye ni makamu wa rais mtendaji wa shughuli za mpira wa vikapu kwa upande wa NBA Minnesota Timberwolves, kuhudumu katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Athletic - Subscription Required)

Newcastle United wanamfuatilia beki wa kulia wa Chelsea Josh Acheampong mwenye umri wa miaka 18 na wanaweza kujaribu kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 19. (gazeti - Subscription Required)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’