Azam Fc yafafanua hatma ya Fei Toto

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Sep 2024
Azam Fc yafafanua hatma ya Fei Toto

Baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa kiungo wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto' amegomea mazungumzo ya mkataba mpya, Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' amesema anaamini Fei Toto ataendelea kusalia Azam Fc na hata kama akitaka kuondoka klabu haitamzuia

Kumekuwa na taarifa kuwa Fei Toto kwa sasa hana furaha ndani ya Azam Fc na yuko tayari kusaka changamoto mpya kwingine pale msimu huu utakapomalizika

"Fei hajacheza Azam muda mrefu, ana miaka miwili kwenye mkataba wake uliobaki. Kuna wachezaji kwenye mikataba yao ina miaka miwili ambayo ni mkataba wa Fei uliobaki"

"Hayo yanayosemwa Fei amegoma kusaini mkataba, ni maneno ya watu; ujue Feisal sasa hivi ni staa mkubwa kwa hiyo lazima azungumzwe ili mtu apate engagements"

"Halafu Fei kuondoka Azam ni kitu kinachowezekana, hatujawahi kuzuia mchezaji kuondoka, wala hatuwezi kumuuliza kwa nini unaondoka?"

"Fei alikuwa Azam alipokuwa mtoto, kisha baadae akarudi. Fei anataka kubaki Azam FC kwa sababu yeye mwenyewe amechagua kuja Azam FC. Tukisema tunaweka kambi kwanzia tarehe 10 yeye anakuja tarehe 8," alisema Zakazakazi

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’