Tumpe muda Mutale - Ahmed

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th September 2024


Tumpe muda Mutale - Ahmed

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema winga Mzambia Joshua Mutale anahitaji muda kuwadhihirishia Wanasimba ubora wake

Kwa siku za karibuni, Mutale amekumbana na ukosoaji kutoka kwa mashabiki wa Simba wengi wakiamini anahitaji kubadilika kwani aina yake ya uchezaji haisaidii Simba

Hata baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahli Tripoli uliopigwa Libya, Mutale hakuwa katika kiwango bora hivyo kumlazimu kocha Fadlu Davids kumtoa katika kipindi cha pili

Ahmed amesema nyota huyo ameyasikia maoni ya Wanasimba lakini ni wazi bado ni mapema kumkatia tamaa, atahitaji muda ili kudhihirisha kwa nini Simba ilifunga safari Zambia kumsajili

"Ni kweli Joshua Mutale mchezo ulimpalia kabisa na hata ukiangalia kipindi cha pili alipata nafasi na kushindwa kuitumia baada ya hapo ilimuondoa mchezoni kwa dakika zote 90"

"Si hivyo tu kitu ambacho anachofanya Mutale bado Wanasimba hawajaridhika kutokana na ubora wake. Watu wanaufahamu ubora wa Mutale tuna matarajio nae bado ni mechi chache tumpe muda atakuwa sawa na tutafurahia matunda yake," alisema Ahmed katika mahojiano na Crown Media


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.