Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Septemba 21 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Septemba 21 2024

Miamba watatu wa Ulaya wanataka kumsajili Mason Greenwood, PSG wanavutiwa na mshambuliaji wa Newcastle na Chelsea wanataka kumuuza Axel Disasi. Barcelona, Atletico Madrid na Bayern Munich ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji mshambuliaji wa Marseille Mwingereza Mason Greenwood, 22. (Talksport)

PSG wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle raia wa Uswidi Alexander Isak huku Magpies ikiweka thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa takriban euro 100m (£83.8m) (Fichajes - in Spanish)

Chelsea wanataka kumuuza mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la uhamisho la Januari. (Fichajes - in Spanish)

Nottingham Forest inawafuatilia wachezaji wawili wa kimataifa wa Uturuki, winga wa Galatasaray Baris Alper Yilmaz, 24, na mshambuliaji wa Besiktas Semih Kilicsoy, 19. (HITC)

Arsenal walikutana na mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 28, kisha Brentford, majira ya kuchipua - lakini waliamua kutomsajili. Badala yake, alikwenda kwa klabu ya Saudi Al-Ahli. (TBR Football)

Juventus watatafuta kumsajili mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David mwenye umri wa miaka 24 mnamo mwezi Januari kwa mkataba wa euro 15m (£12.5m). (Calciomercato - In Italian)

Real Madrid inafikiria kufikia kiwango cha euro 45m (£37.7m), kipengele cha lazima katika suala la kumuuza beki wa Valencia mwenye umri wa miaka 19 kutoka Uhispania Yarek Gasiorowski. (AS – in Spanish)

Everton itampa mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin fursa ya mwisho ya kusaini mkataba mpya kabla ya mkataba wake kumalizika msimu ujao wa joto, huku Newcastle wakionyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)

Mazungumzo ya mkataba kati ya Southampton na mlinzi wa England Kyle Walker-Peters yamegonga mwamba huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa miaka 27 ukikamilika msimu ujao wa joto. (Fabrizio Romano)

Southampton wamemjumuisha meneja wa Blackburn John Eustace kwenye orodha yao huku Saints wakifikiria nani wa kuchukua nafasi za Russell Martin. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’