Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 23 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 23 2024

Manchester City wako mbioni kumsajili Mjerumani Jamal Musiala, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid kwa kiungo huyo wa Bayern Munich. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin hajakaribia kusaini mkataba mpya zaidi ya msimu ujao na Everton, huku Newcastle United ikiendelea kufuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (CaughtOfisde)

Mkataba wa mlinzi wa Liverpool Trent Alexander-Arnold unakamilika msimu ujao na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, anasema kushinda mataji itakuwa sehemu muhimu ya mawazo yake linapokuja suala la kusaini nyongeza ya kandarasi. (Liverpool Echo)

Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham wote zinavutiwa na mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26. (Teamtalk)

Newcastle ndio klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi ya Premia kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa chini ya miaka 21 mzaliwa wa Marekani wa Italia Luca Koleosho, 20, ambaye pia anawaniwa na klabu ya Burnley. (HITC)

Ligi ya Premia, pamoja na ligi kuu za Ulaya, zinajaribu kukubaliana mpango ambao utamaanisha kuwa usajili ujao wa majira ya joto utafungwa kabla ya kuanza kwa msimu. (Mirror)

Kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter angependa kujiunga na Everton ikiwa nafasi itapatikana. (Football Insider)

Real Madrid wanamfuatilia mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Castello Lukeba, 21. (Marca - kwa Kihispania) Aston Villa, Fulham na Nottingham Forest wanamfuatilia winga wa Galatasaray, 24, Baris Alper Yilmaz, wakati Forest, Brighton na Tottenham wanamnyatia mshambuliaji mwenza wa Uturuki Semih Kilicsoy, 19, ambaye yuko Besiktas. (CaughtOffside)

Wasaka vipaji wa Manchester United, Newcastle na Tottenham walifuatilia mechi ya Jumamosi ya Southampton ambapo kiungo wa kati wa Uingereza Tyler Dibling, 18, aliifungia klabu hiyo. (HITC)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’