Azam - Simba - Local

Azam Fc, Simba hapatoshi New Amaan Complex leo

Joel JJ By Joel JJ
26 Sep 2024
Azam Fc, Simba hapatoshi New Amaan Complex leo

Baada ya kufuzu hatua ya makundi ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika kibabe, Simba inatarajia kushuka ugenini kuwakabili Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Ligi Kuu ya Tanzania Bara imehamia kwa muda Visiwani Zanzibar baada ya wenyeji wa mchezo huo, Azam FC kuchagua kuutumia uwanja huo uliofanyiwa ukarabati hivi karibuni

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amesema hawatarajii mchezo huo kuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wao Azam FC

"Azam ni timu nzuri, wanawachezaji wenye uwezo mkubwa, nadhani utakuwa mchezo mzuri na wenye upinzani," alisema Fadlu. Kocha huyo alisema amekiandaa vizuri kikosi chake kuelekea katika mchezo huo utakaochezwa kuanzia saa 2:30 usiku

"Tumetoka kwenye mchezo mgumu dhidi ya Al Ahly Tripoli, lakini tumefanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huu, ni muhimu sana kwetu kupata ushindi ili tuendelee pale tulipoishia katika michezo yetu ya Ligi Kuu," Fadlu alisema

Naye Kocha Mkuu wa Azam FC, Rashid Taoussi, ambaye atakuwa anakutana na Simba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo alisema amejindaa vizuri kuwakabili Wekundu wa Msimbazi ingawa amekiri anatarajia mchezo utakuwa mgumu

Taoussi alisema ugumu wa mechi hiyo unatokana na aina ya mpinzani wanayetarajia kukutana naye

"Yote kwa yote tumejiandaa vizuri, tunataka pointi tatu ingawa mchezo hautakuwa mwepesi, wachezaji wangu wapo tayari kwa ajili ya mchezo huu muhimu," alisema Taoussi

Kocha huyo ameanza kuifundisha Azam FC hivi karibuni akirithi mikoba iliyoachwa na Yousouph Dabo, ambaye aliondolewa kutokana na matokeo yasiyoridhisha

Azam yenye maskani yake Chamazi, imecheza mechi nne na imejikusanyia pointi nane wakati Simba yenye pointi sita imeshuka dimbani mara mbili tu

IPP Media

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
5h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
6h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
8h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
8h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
9h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
9h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
10h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
12h ago
READ MORE →