Baada ya kuifungia Yanga goli pekee la ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KenGold hapo jana, beki Ibrahim Bacca amesema huo ni mwanzo tu kwani msimu huu amejiwekea malengo makubwa
Bacca alifunga bao hilo dakika ya 13 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa Stephane Aziz Ki ambaye ameandikisha 'assist' yake ya pili msimu huu
"Nafurahi nimeifungia timu yangu bao la ushindi siku ya leo. Mchezo ulikuwa mgumu lakini muhimu kwetu tumefanikiwa kuibuka na ushindi"
"Huu ni mwanzo tu, msimu huu nina 'target' ya kuwania kiatu cha dhahabu, hakuna kisichowezekana" alitamba Bacca baada ya kupewa taarifa kuwa wanaoongoza katika orodha ya wafungaji msimu huu wana mabao mawili
Bao alilofunga Bacca jana limeingia katika vitabu vya kumbukumbu kwani hilo ni bao lake la kwanza tangu alipojiunga na Yanga misimu mitatu iliyopita