Simba yamnasa Mpanzu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st October 2024


Simba yamnasa Mpanzu

Simba imetambulisha usajili wa winga Mcongomni Elie Mpanzu aliyetua kutoka klabu ya AS Vita

Lilikuwa ni suala la muda Simba kuthibitisha usajili wa nyota huyo ambaye wiki iliyopita alikuwepo nchini kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho la CAF kati ya Simba dhidi ya Al Ahly Tripoli

Ujio wa Mpanzu wa unakwenda kuimarisha eneo la safu ya ushambuliaji ya Simba kwani anaweza kutumika kama winga au namba 10

Mpanzu ataanza kujifua mapema na Simba huku akisubiri kufunguliwa kwa Dirisha dogo la usajili Disemba 15 aanze kutumika rasmi kwenye ligi

Nyota huyo amepewa mkataba wa miaka miwili


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.