Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 03 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 03 2024

Arsenal, Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid wako mbioni kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen msimu ujao, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka €150m (£125m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Bild – in Deutsch)

Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe na meneja wa zamani wa Chelsea Graham Potter ni wawili kati ya wachezaji wanaowania kuchukua nafasi ya Erik ten Hag iwapo ataondoka Manchester United, huku meneja wa zamani wa England Gareth Southgate na mkufunzi wa Inter Milan Simone Inzaghi pia wakiwa kwenye mfumo. (TeamTalks)

Lakini, ripoti kutoka Italia zinasema kuwa meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri anapendelewa na Sir Alex Ferguson kuwa meneja ajaye wa Manchester United. (Express)

Meneja wa Southampton Russell Martin yuko kwenye hatari kubwa ya kupoteza kibarua chake kufuatia timu yake kuanza vibaya msimu huu. (Mirror)

Meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard amedokeza nia yake ya kuwa meneja wa England, ambayo kwa sasa inashikiliwa na meneja wa muda Lee Carsley. (Football London)

Kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25, anasema hajutii baada ya kukataa kuhamia Liverpool katika dirisha la usajili la kiangazi. (Mirror)

Winga wa Borussia Dortmund, 22, Karim Adeyemi analengwa na Liverpool. Klabu hiyo ya Merseyside inamtaka mshambuliaji huyo wa Ujerumani kuchukua nafasi ya Mohamed Salah msimu ujao. (Sun)

Everton hawana wasiwasi kuhusu mpango wa dirisha la uhamisho wa Januari kutoka kwa wapinzani wao Liverpool kumnunua beki wa kati wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22. (Liverpool Echo)

Everton wanaweza kufufua nia yao ya kumnunua fowadi wa Paraguay Miguel Almiron, 30, ambaye huenda akaondoka Newcastle United mwezi Januari. (TeamTalks)

Manchester United wanaweza kuchagua kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa beki wa Uingereza Harry Maguire, 31, ambaye anafikia kikomo mwishoni mwa kampeni za 2024-25, kwani wanataka kumzuia kuondoka akiwa huru. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’