Kibu hana hofu na usajili wa Mpanzu Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd October 2024


Kibu hana hofu na usajili wa Mpanzu Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba Kibu Denis amemkaribisha winga mpya wa timu hiyo Elie Mpanzu ambaye juzi usiku Simba ilithibitisha kukamilisha usajili wake kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya AS Vita

Kibu amesema ujio wa Mpanzu utaongeza ubora katika safu ya ushambuliaji kwani kocha Fadlu Davids atakuwa na wigo mpana wa wachezaji wa kuwatumia katika eneo la winga

Hata hivyo amesema ataendelea kupambana katika kiwanja cha mazoezi ili kuhakikisha anampa kocha sababu ya kuendelea kumtumia

"Namkaribisha sqana Mpanzu Simba, nafahamu ni mchezaji mzuri ambaye ataongeza kitu katika timu yetu"

"Binafsi napenda ushindani kwani utafanya niongezee bidii ya mazoezi ili kumshawishi kocha kuendelea kuniamini kunipa nafasi ya kucheza"

"Hata ningeletewa Cristiano Ronaldo wa Al Nassr, bado ningefurahia kucheza naye, kwani ubora wake ungenifanya kutamani kujifunza vitu vya kunifanya kocha aone umuhimu wangu kikosini," alisema Kibu

Baada ya usajili wa Mpanzu, katika eneo la washambuliaji wa pembeni, Simba sasa itakuwa na machaguo zaidi Mpanzu akiungana na Kibu, Ladark Chasambi, Saleh Karabaka, Edwin Balua na Joshua Mutale

Kibu, Mutale na Balua ndio waliopata nafasi zaidi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Fadlu


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.