Klabu ya Yanga iko katika mchakato wa kunasa saini ya kiungo mkabaji mpya, Charve Onoya, kutoka AS Maniema ya nchini DR Congo
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema mchezaji huyo ni mmoja ya watakaovaa uzi wa kijani na njano kipindi cha dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba, mwaka huu na Januari, mwakani
Yanga inataka huduma ya mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha eneo lao la kiungo, ambalo kwa sasa linaongozwa na Mganda Khalid Aucho na Aziz Andambwile
Kiungo huyo nusura ajiunge na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, lakini dili lilifeli, na safari hii mabosi wa klabu hiyo wamerejea kwa nguvu zote
"Kwa sasa tegemeo ni Aucho, na anaonekana amechoka kutokana na kucheza michezo mingi, anahitaji msaidizi, Mudathir yeye anapewa kazi ya kwenda kushambulia mianya inayoachwa na wapinzani, mara chache anakuja kumsaidia. Andambwile bado hana uzoefu, tuna michuano mingi migumu ya kimataifa, kwa hiyo lazina tupate kiungo mkabaji mzuri na mwenye uzoefu, tumeangukia kwa huyo jamaa Mkongomani," kilisema chanzo kutoka Yanga