Baada ya kuanza msimu kwa kusuasua, KenGold jana walizinduka na kuhesabu ushindi wa kwanza msimu huu kwa kuwachapa maafande wa JKT Tanzania kwa bao 1-0
Bao hilo pekee la mchezo wa awali wa Ligi Kuu leo uliofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya limefungwa na Hebert Lukindo katika dakika 68
Ken Gold imepoteza michezo 5 ya kwanza ya ligi hiyo na imetoka sare mchezo mmoja
Aidha matokeo ya mechi nyingine, Simba na Coastal Union zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa KMC Dar es Salaam wakati Mashujaa ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Singida Black Stars kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
Singida BS imeendelea kuongoza ligi ikifikisha alama 16, ikifuatiwa na Simba na Fountain Gate ambazo zina alama 13 kwa kila moja huku Yanga ikiwa ya nne ya alama 12



