Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imewasili Kinshasa, DR Congo tayari kwa mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afcon 2025
Stars inayoshika nafasi ya pili kundi H ikikusanya alama nne, itashuka dimbani Pentecost Martyrs kesho Alhamisi katika mchezo dhidi ya DR Congo ambao utapigwa saa 1 usiku
Ni mechi muhimu kwa Tanzania kupata ushindi au hata alama moja ugenini ili kuweka hai matumaini ya kufuzu Afcon
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo jijini Dar es salaam katika mchezo mwingine ambao unaweza kutoa taswira ya mwelekeo wa kundi H



